Kuna baadhi ya makabila hapa Tanzani wanaamini ugomvi katika mahusiano ni sehemu ya upendo, sijui kama ni kweli juu ya imani hii. Japo zipo sababu mbalimbali zinafanya mahusino mengi kutumbukia kwenye ugomvi katika mahusiano ya kimapenzi na sababu hizo ni pamoja;
Masuala ya Fedha
Japokuwa fedha si msingi wa mapenzi, lakini ni kitu ambacho kinahitajika sana katika maisha ya kila siku ya kila mtu na ya familia. Na kimekuwa ni mojawapo ya vitu ambavyo wapenzi katika mahusiano au ndoa hugombana sana juu yake.
Mwenza mmoja anapokuwa mtumiaji mbaya wa fedha na mwingine siyo, huibua malalamiko na ugomvi. Baadhi ya wapenzi hasa wanawake hawataki kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mahitaji ya msingi ya nyumbani na badala yake kuwaachia mzigo mkubwa wanaume.
Hili linaibua malalamiko mengi kwa baadhi ya wanaume,na wakati mwingine toka kwa wanawake. Matumizi makubwa ya fedha kwaajili ya pombe na sharehe nyingine kwa wanaume na baadhi ya wanawake kumekuwa mojawapo ya sababu za ugomvi juu ya fedha katika mahusiano.
Ni muhimu kwa wenza wawili kupanga jinsi ambavyo fedha zao zitapatikana na kutumika. Vipaumbele vya kufanyika kwanza na kiasi cha kutumika kwajili ya starehe na urembo kwa wanawake kwa mfano.
Suala la Unyumba
Japo kuwa suala kufanya mapenzi si kila kitu kwa wapenzi ndani ya nyumba lakini linachangia sana katika kuleta ugomvi aina yao. Kufanya mapenzi kupita kiasi au mara chache kunaleta matatizo kwa wapenzi hasa ambao wana uhitaji tofauti.
Wengine wanaona kama mpenzi ambaye hahitaji kufanya mapenzi mara nyingi na mwenzake labda anauhusiano na mtu mwingine zaidi yake. Au hamvutii tena kama zamani na huenda akaanza kuangalia nje.
Hii inajenga kutojiamini na kupoteza uaminifu,ambalo ni tatizo jingine kubwa katika mahusiano kama tulivyoonesha mwanzoni.
Vipaumbele katika Maisha
Wapenzi wawili wanapokuwa na mipango na malengo tofauti ni tatizo kubwa. Watu wanapokuwa katika uhusiano ambao ni wa kuishi daima,malengo na vipaumbele vyao ni lazima vioanishwe na juhudi za kila mmoja zilenge katika kufanikisha mipango hiyo ya pamoja.
Kunapotokea kuwa kila mmoja ana malengo tofauti basi hata vipaumbele vitakuwa tofauti na hapo ndipo shida zinapoanzia.
Uaminifu
Uaminifu katika mahusiaono ni jambo la muhimu sana. Bila uaminifu ni ngumu sana kwa mahusiano yoyote kudumu.
Uaminifu ni kitu ambacho hujengwa kwa muda mrefu na kikipotea ni ngumu sana kukirudisha. Japo inawezekana kujenga upya uaminifu lakini huchukua muda mrefu sana.
0 comments:
Post a Comment