juu

Tuesday 4 June 2019

SABABU ZA WANAUME KUCHAPIWA WAKE ZAO NA RAFIKI ZAO HIZI HAPA





UNAPOKUWA umeingia kwenye ndoa na mwanamke, utambue ana wanaume wengi wanaomtaka lakini huenda anawaka­talia kwa kuwa yuko na wewe. 
Lakini endapo mwanaume atakuwa haoneshi kumjali, ni vigumu sana mke kuendelea kuwa muaminifu na katika mazingira hayo ndiyo unaweza kusikia, mke katembea na shemi yake au mtu mwingine. Hata hivyo, najua wapo wanaojiuliza sababu hasa za mke kufikia katua ya kuchepukia kwa rafiki wa mume wake. Nimechunguza na kubaii baadi ya sababu kama zifuatazo hapa chini;
Moja; endapo utakuwa umeingia kwenye ndoa na mtu, wewe mwenyewe unaweza kutengeneza mazingira ya kusalitiwa. Usipoonesha kumpenda, kumjali, kuthamini penzi lake kisha rafiki yako akayaonesha hayo kwake, ni rahisi sana kukupiku. Kwa mfano, endapo umeoa lakini hata siku moja hujawahi kumpa zawadi au kumtoa ‘out’ mkeo, siku shemeji yake (rafiki yako) akiamua kufanya hivyo, mkeo atahisi yeye ni mtu sahihi kwake.
Mbili; Wapo ambao wanatembea na mashemeji zao kwa sababu tu ya kujirahsi kwao. Kwa mfano unapopendelea kuzungumza mambo ya chumbani na rafiki wa mpenzi wako unatarajia nini? Unapomvalia kihasara rafiki wa mpenzi wako lengo linakuwa ni lipi?
Mbaya zaidi ni pale utakapokuwa na mashemeji ambao hawabipiwi. Hapa namaanisha wale ambao wakiona dalili ya kupendwa tu, wanaomba chansi.
Tatu;Haishauriwi kumuamini sana rafiki yako kwani wengine wakipewa uhuru wa kuwa karibu na mashemeji zao, huchukulia kama fursa ya pekee.
Kwa mfano, unapomuamini rafiki yako kiasi cha kumruhusu aende na mpenzi wako baa, klabu au ufukweni ni kujitafutia matatizo. Tunajua kwamba wapo marafiki waaminifu lakini tambua tu kwamba wengi wanapokuwa mazingira hayo ndipo huishia kusaliti na wakati mwingine bila kupenda.
Kwa nini nasema bila kupenda? Chukulia umemruhusu mpenzi wako aende baa na rafiki yako, wamekunywa pombe hadi wamelewa kisha rafiki yako anamchukua mpenzi wako kwenye gari kumrudisha nyumbani. Wengi kwenye mazingira hayo uzalendo unawashinda. Kwa hiyo kama hutaki yakukute ya kusalitiwa, kama una tabia ya kumruhusu mpenzi wako kwenda baa na shemeji yake, acha mara moja.
Nne; unaweza kuwa na rafiki lakini kumbe ni mnafiki. Huyu ni yule ambaye mko pamoja lakini anajiapiza kwamba siku moja lazima atakuchukulia mpenzi wako. Huyu ndiye tunamuita rafiki mnafiki.
Kutokana na tabia hizo ndiyo maana matukio ya baadhi ya wanaume kuwatongoza wapenzi wa marafiki zao yamekuwa yakiongezeka. Pia wanawake wengi sasa hivi hawaoni hatari kuwatongoza marafiki wa wapenzi wao au wapenzi wa mashoga zao.
Tano; Endapo utagundua mpenzi wako katembea na rafiki yako, kuna uwezekano ameshawishiwa kwa pesa au mali. Hii ni kwa sababu wapo watu ni dhaifu sana, yaani wao kusaliti wapenzi wao kwa sababu ya pesa, mali au tamaa zao za kimwili siyo kitu kigumu.
Ndiyo maana tunashauriwa kuwa na wapenzi ambao hawana tamaa za kijinga. Katika siku za mwanzo za uhusiano wenu ukigundua uliye naye si mtu wa kuridhika na penzi unalompa, pesa na mali mlizonazo, mapema muonesha mlango wa kutokea kwani itakuwa siyo jambo la ajabu kusikia katembea hata na ndugu au rafiki yako.





Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger