UNAJUA kila mmoja anamahitaji mahusiano yake ya kipekee yanayomuelezea yeye kuwa ni mahusiano gani alionayo na binadamu tunahitaji kuelewana , lakini ukweli ni kwamba , kukosekana kwa mahusiano mazuri humaliza akili za watu na nguvu pia. Hasa pale panapokuja swali gumu la mawasiliano.
Sasa leo tuzungumzie suala la mawsiliano katika mahusiano Inabidi kujifunza kuwasiliana ambapo ndio njia nzuri ya kutengeneza mahusiano bora . hebu tuone njia hizi za ufanisi wa mawasiliano katika mahusiano
Kitu cha kwanza Jifunze kutulia. Mruhusu mtu unaewasiliana nae kuongea jinsi anavyojisikia, na atoe mawazo yake bila ya wewe kumuingilia.
Pili Jifunze kuwa msikilizaji mzuri. Yaan jifanye kama wewe umealikwa , na unataka kuwasikiliza watu wanaowasiliana. lakini usije ukakaa tu bila ya maswali. jitahidi kuuliza maswali kadhaa ili kuongeza hari ya huyo mzungumzaji aendelee kuongea
Tatu Usipanic, usifanye papara. Hapa namaanisha kwamba usiingilie muda, subiri mpaka huyo mtu amaliza kuongea na kujieleza. kama utaona bado hayuko tayari kusikiliza, we endelea kusubiri tu.
Nne Usijaribu kuongea juu ya mtu mwingine. usijaribu kuongea juu ya mtu mwingine, yaani mtu anaongea na wewe unaongea , usifanye hivyo. hatakujibu labda awe ni mtu wa ovyo,
MWISHO Usihofie ukimya wa muda.
wakati wa ukimya ndio wakati mzuri wa mawasiliano, hata hivyo katika hali nyingi za mawasiliano ya ukimya unawafanya watu wasijiamini na wasitulie.
Vilevile kuna watu wanahitaji ukimya ili waweze kukusanya mawazo yao na waweze kuongea kitu cha msingi. na wakati huo wa ukimya unatakiwa kuwa msikilizaji mzuri zaidi ya wakati wa kuongea.
0 comments:
Post a Comment