Mapenzi ni kitendawili lakini ukiyapatia yanaweza kuwa matamu sana. Lakini mapenzi yanahitaji kazi unahitaji kujitahidi kuyajenga kila siku ili yasiyumbe wala kubomoka hasa ukiwa kwenye ndoa au mahusiano.
Mkiwa wawili kwenye mahusiano kwa muda mrefu suala la kuchokana lipo na ni muhimu sana kuhakikisha jambo kama hili halitokei kwenye mahusiano yako kwani mkishaanza kuchokana ndio utakuwa mwisho wenu.
Leo tutaangalia mbinu mbali mbali zitakazokusaidia kuhakikisha kuwa mapenzi yenu hayachuji na njia utakazotumia kuhakikisha unakoleza mapenzi ili yazidi kuwaka na kuchanua.
Ili Mahusiano yoyote yadumu ni unahitaji kuyafanyia kazi na uvumilivu ni muhimu sana zifuatazo ni njia na mambo muhimu ya kufanya ili mpenzi wako azidi kukupenda;
1. Kujiamini ni muhimu
Hakuna kitu kinachomvutia mwanaume yoyote kama mwanamke ambaye anajiamini na imara, yaani mwanamke ukianza kujiamini na uzuri wako na imani yako basi mwanaume atazidi kuvutiwa na ujasiri wako na akili yako.
2. Kuwa msikivu na mwenye huruma
Ili kumuelewa mpenzi wako inabidi uwe msikivu, kumsikiliza mtu ndio njia pekee ya kumwelewa. Usikimbilie kumkosoa pale tatizo linapotokea kwa kufanya hivi utaweza kumwonyesha kuwa wewe sio tu mpenzi wake bali rafiki pia.
3. Mthamini Mpenzi wako
Kwenye mapenzi ni lazima kila mmoja amthamini mwenzie kwa njia hii utamuonyesha kuwa unatambua mchango wake kwenye maisha yako na kitu kingine usije ukajaribu kumbadili mpenzi wako ili awe utakavyo wewe bali mthamini kwa vile alivyo kwani ndivyo ulivyompenda.
4. Jifunze vitu vipya kila siku
Ili mapenzi yenu yasichuje basi lazima yaende na wakati ni muhimu kubadilika ili kuwe na hamu fulani mabadiliko haya yanaweza kuwa katika mambo yenu ya chumbani au hata vitu vya kufanya kama kuangalia movie labda au hata kusafiri sehemu mpya.
5. Kuwa mpenzi bora lakini zaidi rafiki wa kweli
Wapenzi ambao wana uhusiano mzuri ni wale ambao pia wana ukaribu wa kirafiki ili wewe na mpenzi wako muweze kudumu zaidi na kupendana ni lazima muwe marafiki hii itawasaidia kuwa karibu zaidi na kuwa wawazi kwa chochote kitakachotokea.
0 comments:
Post a Comment