Sio kweli kuwa watu wanaokaa muda mrefu katika mahusiano ndio wanaweza kukumbana na uhatari katika mahusiano , wapo ambao wamekuwa wakianzisha mahusiano kwa maslahi yao binafsi lakini wenzi wao wanapata tabu kujua kwa sababu wanakuwa tayari wameshapenda.
Hata kama mmekuwa na mahusiano kwa muda wa wiki moja tu, ni lazima kuwa mwangalifu na mtu unaeingia nae katika mahusiano ili kujua kama uko kwenye hatari ya kuumia kwa namba yoyote ile.
Watu wengi hawataki kuamini kuwa kule wanakopenda kunaweza kuwa na hatari ya kuumia , wengi wanaamini kuwa kama mtu anaweza kukuonyesha kukupenda hasa kwa maneno basi anakuwa tayari ameshachanganyikiwa na hakuna kitu unaweza kumwambia , lakini kumbe kuna mazingira yanaweza kuchunguzwa taratibu na ukagundua baadhi ya vitu kama.
Uthibiti usio wa kawaida (Over Control )
kuna watu katika mahusiano haoni kama mwenzake ana thamani kama inavyopaswa kuwa, yeye anataka kuwa muamuzi wa mwisho katika kila kitu, anataka awe msemaji wa mwisho kwa kila kitu, na kama utabisha basi mnaweza kukaa bila maongezi mpaka atakapojisikia kukusemesha wewe.Mfano yapo mahusiano ambayo , mmoja kati yenu anataka kuwa anajua kila kitu kuhusu mwenzake lakini sio vyake, atataka yako simu ajue ni nani anapiga au kutuma sms, atataka kujua unaongea na nani na kwanini.Hii sio dalili ya mahusiano mazuri.
kujipendelea (self-centeredness)
Hakuna maana ya mapenzi kama mwenzi wako anakuwa akijali nafsi yake kuliko yako, maana ya mapenzi ni kujitoa muhanga kwa kila kitu , mapenzi mazuri ni yale ambayo kila upande unakuwa ukifaidi kile mlicholenga kukianzisha , lakini kama mmoja ananungunika na mwingine anafurahia na kuona sawa tu basi hayo sio mapenzi, ONDOKA HARAKA.
Kutaka kujimilikisha
Hatukatai kuhusu kumpenda mtu mpaka kumuonea wivu, lakini kuna ule wivu tunasema ni ujinga, wivu ambao anataka kujimilikisha wewe kuwa ndio wake kwa kila kitu.Wivu ambao kila sehemu na kila kitu chako basi ni lazima kipitie kwake, hii inachosha na kumfanya mmoja wenu akose amani ya maisha na mapenzi pia.
Ukosefu endelevu.
Kuna mtu anaweza kuwa amekuchoka lakini hataki tu kusema kwa sababu hataki kuwa sababu ,mtu huyu anaweza kuwa ni mwenye vituko na makosa ya kila siku yanayojirudia kila mara na kukufanya kuchoka.Fikiria kwamba amekuwa kila siku akifanya kosa moja ambalo kwa namna moja ama nyingine ameshajua kuwa linakukwaza , lakini cha ajabu kwa sababu ya mapenzi akiomba msamaha Unakuwa laini, Amka na anza kuchukua hatua hapo.
Udanganyifu uliopitiliza.
Ujawahi kusikia kesi ya kuwa mtu anakuwa akifanya kitu sio kwa sababu akili yake inataka afanye kitu fulani, lakini kwa sababu ya ushawishi kutoka kwa mtu anaempenda anajikuta anaweza kufanya chochote tu , hii utokea sana katika mahusiano ya sasa, mmoja wenu anakuwa na maneno ya kukulaghai na kukufanya ukubaliane na kile anataka yeye wakati mwisho wa siku kitawaingiza katika matatizo tena hasa kwa upande wako.
NB;-Hakuna mtu asiependa amani kwa kila kitu, kuwa kwenye mahusiano au kuwa na mtu unaempenda kusikufanye ukaona kuwa maisha hayana maana kabisa, unachopaswa kujua ni kwamba , pale unapoamua kuwa katika mahusiano kitu kikubwa cha kuzingatia ni amani ya moyo wako , hivyo tafuta mahusiano yenye afya sio kupelekwa tu kwa sababu unahitaji mahusiano.
0 comments:
Post a Comment