juu

Saturday 30 November 2019

Jinsi gani ya kuongea na msichana bila kupungukiwa Swaga




Jifunze jinsi ya kuongea na msichana bila kupungukiwa na swaga, bila ya kujali upo wapi. Unachohitaji ni hivi vitu 10 hapa kufanya maajabu na kumteka!.
Mfate alipo

Moja ya vitu ambavyo ni vigumu kwa wanaume wengi kufanya ni kumfata msichana anayemtaka kwa mara ya kwanza.

Kuchati na mwanamke ni kitu rahisi sana hatakama hamkuwahi kuonana, lakini kumfata ndipo kwenye utata.

Wakati unapohitaji kumfata msichana ambaye haukuwahi kuongea nae kabla, na ukahitaji kuanzisha maongezi, moyo huanza kwenda kasi kama ngo'ombe anayekwenda machinjoni.


Fata hizi hatua 10 kwa uda huu mfupi, na kabla haujafika huko, kujua jinsi ya kuongea na mwanamke unayemtaka itakua rahisi kama vile mtu anayetembea kwenye bustani.
Unapenda sana kuongea na wanawake wa hadhi(high status), si ndiyo?
Kama vile upendavyo, vivyo hivyo wanawake hupenda kuongea na wanaume wa
viwango.
Kwa maana hiyo, hakuna cha kuogopa hapa!.
Kumbuka, sheria kubwa ya kuijua wakati unataka kujua jinsi ya kuongea na mwanamke unayemtaka - hautakiwi kuvuka hatua. Kama ulivyojifunzaga kutembea kabla haujajua kukimbia, unatakiwa kujua jinsi ya kumtamanisha hata kabla haujaongea nae.

Sasa Twende..

# 1Mfanye ajue kuwa unamtaka. Najua unajua, kuongea na mwanamke kwa mara ya kwanza siyo kama mtu anayemfata mwanamke na kumuomba watoke out. Inatakiwa iende kwa hatua, lakini licha ya hiyo hautafikia lengo. Mwanamke anahitaji kujua unamtamani/ kumpenda hata kabla hamjaongea ili aweze kukuchambua / kukufahamu / kukuchunguza(to evaluate you).

Kama utamfata mwanamke ambaye kwanza hajawahi hata kukuona ukionesha interest kwake, utaishia kumshtua tu. Na ataishia kukwambia neno ambalo mama yake alimfundisha akiwa mdogo - kwamba akikutana na mwanaume amwambie nini "Niache".

.

#2 Fanya mautundu. Baada ya kujua kuna kiumbe kama wewe duniani, anza michezo ya kichokozi. Jitahidi kuwa unamuangalia kila wakati mpaka yeye ajue unamuangalia, hii itamfanya naye awe anafanya hivyo hivyo japo hatapenda kujionesha(ila usimshangae). Sasa unatakiwa kujua, na yeye anakuangalia? je marafiki wake wanakuangalia? je wanatabasamu wakikuona?. Jaribu kujua hayo.


Hakuna haja ya kutaka kujua jinsi ya kumfata mwanamke ambaye ukimtazama anakuangalia vibaya au kwa hasira, na wakati mwingine hajali kama unamuangalia au la. Kumbuomba mwanamke kutoka nae mda mwingine huwa kama majanga kama haujamvutia, hivyo kuwa mwangalifu.

#3 Usimchomoe au kumuita kutoka mahali. Kumchomoa mwanamke kutoka sehemu fulani mara nyingine huwa smart na ya kuvutia, lakini mara nyingi siyo njia sahihi. Jitahidi kuangalia mazingira.
Mfano kama alikua sehemu fulani, kisha akawa anaondoka unaweza mfata na kusimama mbele yake na kumuabia vitu kama " natamani ungejua ni kwa muda gani nimekua nikitamani kuwa na muda kama huu". au kitu kingine cha kawaida. Iwe ofisini, park ya magari au hata bar, jaribu kumuuliza swali ambalo linaendana na mazingira.

Lakini kumbuka kutumia lugha ambayo itamchanganya ka kutaka wewe uongee zaidi ili akuelewe.

#4 Usikamie maongezi. Hii hufanikiwa vizuri pale unapomuuliza maswali ya kumchanganya na kuwa anakujibu. Akishakujibu, wote mnakua katika mood ya kuongea lakini bado hamjawa marafiki. Atakuwa anayajibu maswali yako huku akitazama sehemu nyingine. Wakati mwingine anaweza hisi unamtania au unataka kumchanganya, hivyo hatatamani kuendelea na maongezi

Unaweza ukafanya hivi, Jitambulishe wewe ni nani au endelea kumuuliza maswali kisha baadae kidogo jitambulishe. Kwa kuangalia muitikio wake wa maongezi, mwambie ni kwa muda gani umekua ukitamani ukutane nae.

Tayari anajua ni kwa muda gani umekua ukimtazama, kwa hiyo huna haja ya kuigiza kwamba umestukiza.


#5Mpe nafasi. Usimsimamishe maeneo ambayo yatamfanya asiwe anajiamini, mazingira kama vichochoroni au sehemu za kujificha. Kama utaweza, unaweza ukaongea nae hata mbele ya rafiki zake. Kumbuka, ukimsimamisha sehemu ambayo ni salama itamfanya ajisikie kujiamini na kukuamini pia kuwa wewe siyo mtu mbaya.

Baada ya kumchangamsha, sasa atakuwa anatamani aendelee kuongea na wewe zaidi na utazidi kumvutia kiasi kwamba hataweza kutambua kama unamtega ili uwe nae.

Bado tupo njiani, hatujafikia lengo la kuhakikisha swaga hazipungui. Ila hizi tips zinatosha kabisa kumvutia mwanamke na akaanza kuongea na wewe na kupenda kampani yako muda wote.
Sasa soma hizi tips nyingine 5 ujue ni kitu gani utaongea na huyo msichana ili uendelee kumtamanisha aendelee kuongea na wewe kwa vile unavomfurahisha moyo wak
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger