1. Anaporudi kutoka kazini, safarini au kwenye shughuli yoyote iliyowatengenisha, anza kwa salamu nzuri.
2. Unapompokea au kukutana naye basi fanya hivyo ukiwa na uso wa bashasha.
3. Vaa mavazi nadhifu. Jipambe na upake manukato kwa ajili yake.
4. Unapoanza kuzungumza naye anza na mambo au taarifa nzuri, na kama kuna taarifa mbaya subiri mpaka atakapopumzika.
5. Mpokee kwa maneno ya upendo na lugha ya kumpongeza au kumpa pole au lugha yoyote inayoonesha kumhurumia kwa kazi za kutwa nzima.
6. Ipendezeshe na uilainishe sauti yako kwa ajili ya mumeo, usifanye hivyo mbele ya wanaume wengine.
7. Utunze mwili wako na kujiweka katika hali ya umaridadi na muonekano mzuri.
8. Tumia manukato, rangi na mavazi yanayopendelewa na mumeo.
9. Jitahidi mara kwa mara kubadili mtindo wa nywele, manukato na kadhalika. Lakini usizidishe kiwango, na ufanye hivyo kwa mumeo tu.
10. Usichelewe kumpa mahaba pindi mumeo anapojiwa na hisia ya kutaka kufanya mapenzi.
11. Mwambie maneno matamu na yenye mvuto wa mahaba.
12. Ridhika na yale uliyobarikiwa na kukadiriwa na Mungu.
13. Kumbuka kuwa utajiri wa kweli hupatikana katika imani na uchamungu.
14. Usihuzunike kwa sababu mumeo ni masikini au anafanya kazi ya kawaida. Watazame maskini, wagonjwa na walemavu kisha umshukuru Mungu kwa aliyowajaalia.
15. Mhamasishe mumeo kupunguza matumizi na kuweka akiba ya pesa kwa ajili ya sadaka na kuwasaidia maskini na wale wenye dhiki.
16. Kuwa mwenye shukrani kwa mumeo.
17. Ukiwa mwenye shukrani, mumeo atazidi kukupenda na atajitahidi kukufurahisha na kukuridhisha zaidi.
18. Shikamana na mumeo, hususan katika nyakati za shida, dhiki, maradhi au mumeo anapofilisika au anapokuwa hana pesa.
19. Akikosea usihamaki kwa kumfokea au kuzozana naye. Subiri anapokuwa hana ghadhabu na uzungumze naye kwa amani na kwa kauli nzuri.
20 Akiwa na hasira kutokana na mambo ya nje ya nyumba basi subiri mpaka atakapoondokana na hasira hiyo.
21. Usimuulize maswali mengi au kung’ang’ania kutaka kujua yaliyotokea. Mathalan, kuna wanawake wengine wakiona mume ana hali tofauti huanza kusema: Niambie kumetokea nini? Lazima utaniambia kilichokufanya mpaka ukawa na hasira hivyo… unaficha nini? Nina haki ya kujua au kuna mwanamke kakuvuruga?
22. Onesha ukarimu kwa wageni wake kwa kuwaandalia sehemu nzuri ya kukaa, chakula kizuri n.k.
23. Jifunze namna ya kuwalea watoto vizuri na kuwapa mwenendo mwema wa malezi mema.
24. Usitumie fedha zake bila ruhusa yake, hata kama itakuwa kwa ajili ya kutoa sadaka, labda kama una uhakika kwamba ataridhia.
25. Jitahidi kuwaweka watoto katika muonekano mzuri, mavazi safi n.k. Wape chakula chenye virutubisho, zingatia sana afya yao, elimu na maadili mazuri. Wafundishe kuhusu kumjua Mungu na dini yenu kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment