juu

Thursday 28 November 2019

Misemo 10 Ya Mapenzi Ya Kweli




Mapenzi yamekuwa yakiandikwa kila mahali, kwa sababu ni kitu muhimu kwa kila mtu. Inasemekana kuwa mapenzi ni kama Oksijeni, kwamba mtu wakati mwingine hawezi kuishi bila ya hayo.

Wanadamu mara zote wamekuwa wachunguzi kuhusu hiki kitu mapenzi. Kwa nini mapenzi yanasababisha matatizo? Labda ni kwa sababu mapenzi ni rahisi, au ni ya utata. hutokea haraka. na wakati mwingine taratibu na kukua sana na wakati mwingine mtu hukosea na kurudi kutaka msamaha tena. Ni matamu na ni machungu pia. Na kila mara umuhimu upo kwa kila mtu. Kila mtu Anapenda. Upendo ni kitu kinacho tuunganisha sisi wanadamu.

Kila mtu ana historia ya mapenzi siku zote itakuwa ni kitu fulani cha kujiuliza.Kila maoni yaliopo kwenye mapenzi ni ya mtu pekee. na hapa kuna baadhi ya maoni yanayoshikilia ukweli.

1.Kuachana ni kama sikitiko lisilojulikana

Hujawahi kushinda siku nzima na mtu unayempenda ,na baadae kujisikia kama una masikitiko baada ya siku kwisha? Unakuwa hutosheki na huyo mtu. kuachana na mtu unayempenda ni huzuni . unashukuru kwa muda ambao ulikuwa naye,lakini ndani yako unajiona huna kitu, mtupu. muda unapofika. Kitu ambacho kitakupa nafuu ni kufahamu kuwa utamwona tena katika hali ile ile.

2.Mapenzi yanajumuisha roho moja katika tabia ya miili miwili.

Inakuja hio point katika mahusiano, unafahamu kuwa anakufikiria hata kama hajasema neno hata moja. Unaweza kusoma lugha ya mwili wake kwa haraka na kufahamu kuwa hayuko sawa.. utafahamu wakati akiwa na hasira, utafahamu wakati anahitaji mapenzi yako kwa jinsi anavyokutazama. mapenzi yana muunganiko wenye nguvu. na iko hivyo kwa kuwa mmekuwa mtu mmoja sio wawili tena.

3.Mapenzi ni tunda katika somo la kila wakati, liko katika kila mkono wa mtu.

Upenda uko kila mahali, popote ulipo utakufuata tu. unaweza kudhihirika kwa njia tofauti kutegemeana na mila na tamaduni, lakini upendo ni mkubwa na unapatikana katika majira yote.

4.Upendo hautawaliwi, unapojaribu kutawala, unaharibu. unapojaribu kuufungia, utakufungia wewe, utahangaika kila mara. Najua jinsi watu wanavyoelezea upendo, Lakini upendo unatosheleza katika mabadiliko ya maisha.

Ninachojaribu kusema ni kwamba, hata kama hutaki uwepo kwako, utakuja. utakulazimisha kubadilika hata kama hutaki. unapojaribu kufikiria ni kitu gani hiki, utabaki kushangaa.

5.Upendo ni kitu cha Umilele. Vipengele vinaweza kubadilika , lakini sio kiini chake.



Napenda kuona ndoa ambazo zimedumu kwa muda mrefu. hasa ukiwaona watu wenye umri mkubwa , miaka 70 na bado wanashikana mikono. Wanatembea pamoja, na bado wanachart . wamezeeka lakini bado wanaendelea kupendana kila siku. wanafurahi pamoja. miili yao imezeeka lakini mioyo yao bado. Wametunza upendo ndani yao.

6.Hata kama upendo hautoshelezi , kiasi fulani upo.

Unakumbuka wakati ukiwa mdogo , ulipokuwa unaumia goti lako kwa michezo na mama yako anakimbia kukuchukua na kukumbatia, na kusafisha sehemu hio kwa upendo. upendo huo unafanya kila kitu kuwa sawa. upendo hauondoi matatizo, lakini unaleta urahisi wa kushughulikia matatizo.

7.Palipo na upendo kuna maisha.

Upendo hufanya ulimwengu wa mtu kukua.Unapompenda mtu, unataka kushiriki maisha yako na yeye na kumuonyesha kuwa yeye ni mtu muhimu . Upendo huo huo unaweza kuwaweka watu wawili kuwa mume na mke na kuweza kuishi ndani ya chumba kimoja kwa kushirikishana huo upendo. Popote penye upendo utahakikisha kuwa maisha yapo.

8.Upendo sio kitu cha kutafuta, Upendo utakutafuta wewe.



Upo wakati ambao unaweza ukafuta mawasiliano na watu ,kwa sababu ya kuogopa maumivu . Lakini hata ukifanya hivyo bado kuna wakati utahitaji mtu wa kutoka naye, wa kusema naye, wa kula naye. Lakini hata kama hutatafuta upendo. utakuja kwako kwa wakati wake.

9.Upendo ni msamaha usio na mwisho, Ni kitu ambacho kinakuwa tabia yako.

Penda msamaha.Unapompenda mtu, haijalishi wanafanya kitu gani, utamsamehe. Ingawa kuna vitu vingine ni vigumu kusamehe,Utaweka kila kitu nyuma yako. kwa sababu mapenzi ya kweli hayaoni makosa ya mtu yaliopita. Lakini kama mtu anakuumiza kimwili na kiakili hutaweza kumsamehe, lakini bado utahitaji kumsamehe na kusonga mbele, ila sio kwa kuendelea naye .mtu anayekupenda hataweza kukuumiza kiakili na hata kimwili. Kuwa makini katika hili.

10. Upendo ni kama Saa ya kioo, wenye kujazwa na moyo kama ubongo ulio mtupu.

Angalia kila mtu ambaye yupo kwenye mapenzi na jaribu kutazama nyuso zao, kama za kijinga hivi. Tunaonekana kama wajinga tunapokuwepo kwenye mapenzi. Lakini ni bora nionekane dump na kuwepo na furaha ya kutosha na moyo wenye amani kuliko kuonekana mtulivu na kuwa na sehemu tupu ndani ya moyo wangu mahali ambapo palitakiwa uwepo upendo.

Mapenzi yanakufanya ufanye vitu vya kijinga,lakini kuwa mjinga ndani ya mapenzi ni hisia moja kubwa na nzuri.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger