juu

Wednesday 27 November 2019

Unataka Mapenzi Moto Moto Kitandani….Kunywa Uji……



Ni ndoto ya kila mwanamume kuwa bingwa kitandani lakini nyakati zingine ngoma hukosa hata kushika kasi, na kuwafanya wanaume hao kukandamizwa na mawazo
– Watafiti, hata hivyo, wamebaini vyakula fulani ambavyo wanakushauri kuvitumia kuimarisha ngoma

1. Kahawa
Kikombe cha chai ya kahawa huwa na kafeini ambayo huimarisha metaboli ya mwili. Vile vile, hufanya moyo kudunda haraka na kwa nguvu na hivyo kusambaza damu kwa kasi mwilini, hadi kwa mzinga. Haya ni mambo muhimu kwa mwanamume kushiriki mapenzi vilivyo.
Utafiti unaonyesha kuwa kafeini pia humpa mwanamume uwezo wa kudumu kileleni, na hivyo kumwezesha kuhifadhi nguvu za kutumia wakati ngoma inahitaji nguvu mpya.

2. Soseji
Ni muhimu kwa neva za mzinga kuwa ngangari ili kukupa uwezo wa kufanya shughuli kitandani.
Utahitaji kula vyakula vya Vitamini B1, ambazo hupatikana katika soseji ya nguruwe. Iwapo hupendi kula soseji, pata vitamini hizo kwa maharagwe ama mkate ulioundwa kutokana na unga ambao haujakobolewa.

3. Divai
Divai ni kinywaji tosha kuimarisha nguvu za kiume, hususan divai nyekundu. Hii imebainika kutoa virutubishi vya kemikali ya nitric oxide ambayo husaidia kupanua mishipa mikuu ya damu na kuimarisha mtiririko hadi kwa mzinga.
Kemikali hiyo hufanya kazi kama tu Viagra – kupanua kabisa mishipa mikuu ya damu – ingawa tofauti ni kuwa vidonge hivyo husababisha mishipa hata midogo katika eneo la uume kupanuka.
Tahadhari: usinywe glasi nyingi kwani itakuletea madhara.

4. Uji
Uji huchukuliwa kama kinywaji cha watoto, lakini uji uliotengenezwa kutokana na unga ambao haujakobolewa huwa na nyuzi zinazosaidia kuondoa kolestorol kwenye damu.
Damu ikiwa sawa mtiririko ni haraka na mishipa inaweza kustahimili kishindo kinachotokana na shughuli nzima ya ngoma. Iwapo unataka mzinga kusimama wima kileleni, kopo la uji litakufaa!

5. Ndizi
Ndizi hukupa Vitamini B inayokuwezesha kuhifadhi nguvu za kimwili na kukuondolea mawazo. Vile vile, zimejaa homoni za serotonin na potasiamu ambazo zinatumika kuunda homoni za mahaba na ile ya bromelain, ambayo ni aina ya kemikali inayoimarisha mtiririko wa damu mwilini.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger