juu

Saturday, 30 November 2019

Zifahamu njia za kudumisha uhusiano wako


Mahusiano ya mapenzi yamekuwa moja ya jambo linalolalamikiwa sana na vijana wengi huku wengi wakisema katika dunia ya sasa hakuna mapenzi ya kweli huku wengine wakisema usaliti na kuumizana kumekuwa na nafasi kubwa zaidi kuliko wale ambao


wanakuwa na mipango ya dhati na mambo mbalimbali yametajwa kuchangia usaliti ikiwemo tamaa ya pesa na maisha mazuri kwa mabinti, na tamaa ya ngono kwa baadhi ya wanaume.

Kupitia kipindi cha Late Night kinachorushwa East Africa Radio jana walikuwa wakielezea namna ambavyo mtu mmoja mmoja anaweza kushiriki kudumisha uhusiano wake na mpenzi wake katika kufikia malengo ya kuwa kitu kimoja kama mume na mke, na haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki kutoka katika ukurasa wa facebook wa East Afrca Radio www.facebook.com/EARadio wakionyesha ni jinsi gani wao wanashiriki katika kudumisha upendo na kuepusha kusalitiwa na kuachwa kama si kuumizwa moyo.

West Lif Ema Anger: "Kwanza inapaswa umsome mpenzi wako anataka nini na anataka wewe uweje bila kusahau uaminifu na upendo wa kweli kati yenu ili muweze kusihi kwa amani na upendo siku zote"

Hope Chopa Hope Chopa: "Kupendana ,kujaliana ,kusameheana na kusikiliza hisia za mwenzako lakini pia uvumilivu wa hali ya juu na uwazi. Ila cha muhimu ni kumpenda anayekupenda kweli na si yule anayependa kitu kwa maana kikiisha au kisipo kuwepo mapenz hugeuka kero ndani au kati yenu na kupelekea amani na furaha kutoweka kabisaa kwani hali hiyo itapelekea kuacha au kusaliti penzi lenu na mwisho wa siku mkajikuta matatizoni"

Kidoti Tillya: "Ili kudumisha mahusiano ni upendo wa dhati kwa kila mmoja, pili kila mmoja kujalii hisia za mwenzake yakizingatiwa hayo mahusiano lazima yawe strong."

Irinda Marwa: "Nazungumza nae sana haijalishi limetokea tatizo gani tunakaa pamoja, tunaongea tunasikilizana maisha yanaendelea.....Huwa tunazungumza kwa uwazi kabisa kama mtu na rafiki yake na unashangaa hata kama tulikuwa na tatizo kubwa linaisha tukiwa na furaha na amani inarudi kati yetu."
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger