juu

Saturday, 16 November 2019

JE MNAJUA TOFAUTI KATI YA MAHABA NA MAPENZI?SOMA HAPA



Kwa mujibu wa wajuvi wa lugha, Mapenzi ni hisia za upendo kwa mwenza wako na mahaba ni vitendo vya kuyathibitisha mapenzi.


Ni kwamba mapenzi yako moyoni is emotional issue. You love and if you cant express yourself you end up burning inside kimya kimya.

Wakati mahaba ni vikorombwezo vinavyoashiria mapenzi yako kwa mtu fulani.

Kwa mfano labda mwanaune anampenda mwanamke kutoka moyoni.

Anaweza kumwambia na akakubaliwa ombi lake na wakawa na uhusiano.

Lakini kumpenda mtu pekee hakuwi na mvuto bila mahaba.

Mahaba ni kama vitu vidogo vidogo mtu anavyomfanyia mpenzi wake kwa hiyari yake bila shuruti.

Kwa mfano kumnunulia mwenzi wako vijizawadi vya kum surprise, kumtoa out, kumfanyia shopping ya mara kwa mara.

Kufanya matembezi ya jioni pamoja, kwenda ufukweni kupunga upepo pamoja, kusafiri likizo kwenda miji ambayo ina vivutio nk.

Hata hivyo siyo kila mahaba yanaashiria kupendwa. Hapa kuna changamoto hususan kwa wanawake.

Kuna wanaume laghai wakimtaka mwanamke halafu akawa mgumu kukubali ombi lake mwanaume huanza kumfanyia mwanamke mahaba hatari mpaka mwanamke analainika na kuingia mtegoni, mahaba hapo yanatumika kama chambo cha kumnasa mwanamke na siyo ishara ya kuonyesha upendo kwa mwanamke. Akishammega anasepa na kumuacha mwanamke huyo kinywa wazi asiamini kilichomtokea.

Wanaume laghai hutumia mahaba kuwapofusha wanawake wanaojifanya wagumu kupatikana.

Lakini pia…….


Mahaba ni sanaa na ili kuyanogesha Zaidi yanahitaji timing siyo kukurupuka. Mara nyingi mahaba yanataka surprise. Siyo mwanamke anakwambia anaomba umnunulie hereni halafu ukinunua unaita ni mahaba. No no no no….

Au mwanaume anaomba anunuliwe soks na mkewe halafu mwanamke akinunua anasema kamfanyia mpenziwe mahaba. Ni kujidanganya.

Mahaba ni ku add value kwa mwenzi wako.



Kwa mfano wakati wanaume wanapenda kudekezwa kwa kufanyiwa vitu vidogo vidogo kama vile kuandaliwa nguo za kwendea kazini na chai kuwa tayari mapema na vitafunwa maridhawa. Wakirudi kazini wanapokelewa kama wana kijimzigo kwa bashasha, kusaidiwa kuvua nguo, kupewa face towel ya uvuguvugu kujikanda uso ili kuondoa vijikunyanzi vya stress za kazini na kuleta tabasamu. Kuandaliwa maji ya kuoga ya vuguvugu na baada ya kuoga kuandaliwa sharubati ya matunda au chai au kahawa kutegemea mapenzi yake, kuwekewa vijikaranga vya kutafuna au popcorn wakati anapoangalia TV, hivi vyote ni vikorombwezo vya mahaba.

Na kama mwanaume anahitaji kupumzika apewe nafasi siyo kusimuliwa ugomvi majirani.

Mara moja moja mwanaume kufanyiwa surprise ya kununuliwa soks za viatu, handkerchief, boxer, vest nk, hunogesha penzi zaidi.


Wakati wanawake kwa upande wao……

Wanapenda vijizawadi vya urembo na vitu vitam vitam na kutolewa out mara kwa mara au kufanya safari za kutembelea vivutio na mavazi ya gharama ambayo ni unique yaani ya kutafuta kwa tochi siyo mavazi ambayo yamezoeleka kama sare.

Wanawake wanapenda kufanyiwa surprise kuliko wanaume kwa hiyo ukitaka kumfanyia mahaba mwanamke na kama amependa vazi fulani ambalo ameona mtu kalivaa akalipenda usikurupuke kununua siku inayofuata hata kama una pesa, vuta muda asahau kidogo kisha unamletea siku ambayo hakuitarajia tena kipindi ambacho unaonekana huna hela kabisa.

Hapo mwanamke uso wake utapambwa na tabasamu mpaka utashangaa.

Hata hivyo naomba kutahadharisha.

Mahaba yana tabia ya visasi tofauti na mapenzi.

Sijui nimeeleweka au mnahitaji ufafanuzi?




Ni hivi; mahaba yanataka two ways. Kama upande mmoja pekee ndiyo unaotoa mahaba hufikia mahali mtu huyo hisia zinachoka na kuacha kwa kudhani anajipendekeza.

Hata hivyo kauli nzuri ya kubembeleza na kuheshimiana na kuhurumiana ni sehemu ya mahaba.

Lakini pia hata kama mahaba yana two ways lakini upande mmoja hau appreciate na kushukuru au kuonyesha sura ya kufurahia hayo mahaba anayofanyiwa hali hiyo inavunja moyo wa mtoa mahaba na kujikuta akiacha.

Hata hivyo tabia ya mtu kufanya mahaba inatokana na malezi au inaweza ku manifest kwa mtu mmoja mmoja lakini ni very rare cases.

Ipo mikoa au makabila ambayo mahaba ni sehemu ya utamaduni na iko mikoa au makabila ambayo kimila mwanaume kufanya mahaba ni kuonekana kwamba yeye ni dhaifu.

Nitayataja……

Wakati kanda ya ziwa, kanda ya magharibi na kanda ya nyanda za juu kusini wanaume wakikosa sifa ya kuwa na mahaba kwa wenzi wao ukanda wa pwani ikiwemo zanzibar zinaongoza kwa mahaba kwa wanaume na wanawake.

Kule kwetu kaskazini hususan mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ipo shida kwa wachaga na wamasai na wameru lakini wapare wamebebwa katika kuwa na mahaba kwa sababu ya kupakana na mkoa wa Tanga ambao ndiyo unaosifika kwa kuwa na mahaba Tanzania Bara.
Wapare wao wana mahaba japo ni ya kukopa.



Wachaga wao kwa upande wa wanaume wanataka wafanyiwe mahaba na wake zao huku wao wakishindia vitochi na nyama choma.

Lakini katika ngazi ya familia mahaba yanaweza kufundishwa kulingana na malezi ya familia husika bila kujali kabila wala ukanda. Hapa watoto wanaona wazazi wanavyofanyiana mahaba na wao huja kuiga ukubwani.

Lakini kwa wale wenzangu wanaoita soda ya Sprite kwa jina la Supirang’iti wao mahaba ni kichapo tu kwa wake zao…..

Lipo jambo moja kwamba kuna baadhi wa wanawake na wanaume hawajui kuhusu mahaba kwa wenzi wao na kwa bahati mbaya inaweza kutokea upande mmoja usielewe ukadhani mwenzi wake hampendi kwa sababu hamfanyii mahaba ili kunogesha penzi. Ieleweke kwamba mahaba ni jambo la hiyari la mtu mwenyewe kumfanyia mwenzi wake kwa hiyo siyo jambo la kushurutishana.

Wakati mwingine mtu akilazimisha kutaka mwenzi wake amfanyie mahaba anaweza kuonekana kero kwa mwenzi wake na kusababisha visirani katika uhusiano.

Mahaba yananogesha na kudumisha uhusiano au ndoa kwa wapendanao.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger