juu

Tuesday 5 November 2019

Jinsi ya kuongea na mwanamke unayempenda * Bila ya kuwa na Woga

Kama kweli unampenda msichana, lakini unajikuta ulimi mzito au hata wakati mwingine vidole kuwa vizito wakati una chati nae. Hiyo isikutishe, hivi ndivyo unatakiwa uongee na msichana unayempenda.
Tunajua ya kwamba wasichana hupenda mawasiliano mazuri leo na kesho na siku zote, na tatizo kubwa huja katika uwezo wa kudhihirisha kujiamini kwako na kufurahisha kwako hata pale unapoonekana umeshindwa. Kwa hiyo kama unapenda kujua ni jisni gani ukawa mwanamaongezi mazuri kwa msichana unayempenda na kuwavutia wengine kwa namna unavyoonge, tips zifuatazo zitakusaidia kama utazifuata.

Jinsi gani nitaongea na mwanamke ninayemtaka bila woga?

#1 Siku zote kuwa simple na asilia(Usiwe mtu wa maigizo). Ninajua kukutana/ kuongea na mwanamke unayempenda sana kunatisha kwa kiasi chake, japo tunajifanyaga hatuogopi. Lakini
badala ya kuigiza kwamba wewe ni mkimya na kuigiza kufanya maongezi yanayolenga kumvutia,haitakufikisha mbali. Kuwa wewe, akujue wewe ulivyo.
Kumbuka, kuigiza maisha au vitendo ambavyo siyo vyako mwisho wa siku utakuja kuumbuka mana ukweli huwa haujifichi, kwa hiyo, aminii katika wewe, amini unaweza kupendwa ulivyo. Kwa kufanya hivyo utamjengea mwanamke roho ya kukuamini. 
#2 Kuwa mwangalifu na jinsi unavyomfata. Wakati unajifunza namna ya kuongea na msichana unayempenda, unatakiwa ujue utafanyeje au utamfata vipi. Kama wewe ndiye mtu utakayeanzisha mazungumzo naye, usiogope, mfate taratibu na uongee nae kama rafiki yako wakawaida(usifanye mambo kuwa magumu=dont complicate it), ongea naye kama mtu wa kawaida. Kama ukisita, utaoekana mwoga, na kama utamfata kwa makelele mengi na kiukakamavu utamtisha. So kuwa simple.
#3 Kuwa na mvuto. Hapa simaanishi sura. Ili kufanya maongezi kuwa mepesi na kumfata kiurahisi, jiwekee mwenyewe mazingira ya kuwa na mvuto, angalao ule muda unaotaka kumfata au kukutana naye.
Hii inamaanisha vaa mavazi masafi na yakupendeza na uweze kuyapangilia, nukia, uwe na afya njema(uenokane una afya njema), usisahau kujiachia. Kwa kufanya hivyo kutakufanya ujiamini na kukuondolea woga. 
#4 Tabasamu. Tabasamu ni ufunguo wa maongezi yoyote duniani. Tabasamu linasuuzisha moyo, linatuliza, na kufanya maongezi kuwa ya kuvutia/kufurahisha. Hii ni lazima vinginevyo utafeli, ukumbuke, maongezi yenu sio ya ugomvi.
#5 Muda wote hakikisha mnatazamana(Maintain eye contact). Jitahidi iwe hivyo kadri uwezavyo. Usiwe unatizama chini au pembeni, au katika maumbo yake. Kama hauwezi kumwangalia machoni kwa muda mrefu, basi uwe unaangalia lips zake na macho yake. Kumuangalia usoni kunainesha unayaheshimu maongezi na mwaminifu(haujafata kitu kingine ila yeye tu).
#6 Usikae nae karibu sana(Kuwe na nafasi kati yenu). Haijalishi unafahamiana nae au ndo kwa mara ya kwanza kukaa nae, inashauriwa kukaa mbali kidogo wakati mnaongea, kama angalao futi moja a nusu mpaka mbili kati yenu.
Kuwa karibu nae sana kutamfanya asiwe huru na wakati mwingine sio nzuri kiafya, lakini pia kukaa mbali nae ni ishara ya kuwa muoga na kutokujiamini.
#7 Usipende kuwa sana mtawala wa maongezi. Kama unataka kumfurahisha mwenzio katika maongezi, usitawale maongezi – mpe nafasi. Kadri utakavyojifanya kujionesha kwamba unajua kuongea sana kana kwamba utamvutia, kuyatawala maongezi inafanya yaonekani ni ya upande mmoja na hayatafika mbali na utamkera mwenzako. Jitahidi sana kuwe na uwiano katika maongezi yenu.
Ibua mada yoyote itakayowafanya nyie wawili kuchangia na wakati mwingine jitahidi kumhoji maswali yatayomfanya yeye afunguke. Muulize maswali mengi kuliko wewe utavokua unajieleza – mana utamueleza zaidi ya hata vile asivyopenda kusikia.
#8 Tumia Luga nzuri. Hatakama mwanamke unayeongea nae ni muhuni katika lugha yake, bado uunatakiwa kuyachuja maneno yako na tumia lugha ya busara.
Kumjibu au kumuongelesha lugha ya kihuni, au kutumia misemo ya mitaani, kutamjengea maswali mengi kwamba lengo lako ni nini lakini pia atajua kiwango chako cha kuelimika(Intelligence). Kuwa wa viwango ukiyasoma mazingira, usizidishe viwango sana mana unaweza kuboa
#9 Tumia ishara za mikono. Ishara husadifu kilichopo ndani ya kichwa cha mwanaume. Ishara za mikono zinamatumizi mengi. Inaweza kuwa ishara ya kile kinachoendelea kwenye mawazo yako, lakini pia inaongeza ladha ya maongezi. Tumia ishara zitakazoonesha kuwa wewe ni mwema, mwerevu, mwelewa na mwenye kujiamini. Usitumie ishara zinazoweza kuashiria matusi au udhalilishaji.
#10 Mshawishi / Msifie lakini sio sana. Inaweza kupitia vitu vidogo kama nguo aliyovaa, nywele zake, au kitu kingine kutoka kwake ambacho unaweza kumwambia ni cha tofauti kwake ukilinganisha na wanawake wengine. Inashauriwa pia wakati mnaanza maongezi umsifie kidogo hata kwa kukubali kukutana na wewe, ni ishara ya upendo
#11 Luga ya mwili. Hata kama hampo karibu mnatakiwa miili yenu iwasiliane/iseme. Hii inahusisha kugonga tano, kushikana viganja, au hata kumshika bega kama hatojali. Hizi lugha huja tu pale maongezi yanapokua yamenoga – ila usizidishe kumshikashika
#12 Jitahidi maongezi yasikatike. Kuna wakati unajikuta unafuraha kwa uwepo wake, na unajikuta unatamani umtazame tu muda wooote. Kuwa kimya kwa muda fulani kunarudisha maongezi nyuma na unaweza kujikuta unaogopa mpaka unajiuliza ulete mada gani nyingine ya kuvutia, mwisho wake kama hautakua mwangalifu utajikuta na mwisho ambao sio mzuri. Badala yake…..
a)Uliza maswali – maswali ambayo yanaonesha unapenda kazi/ shuguli zake.
b)Ingiza utani – hapa inafufua mood na inachangia kuibua mada mpya.
c)Ibua maswali yasiyo na majibu ya moja kwa moja – yakwepe maswali yenye majibu ya ndio au hapana.
#13 Mchangamshe kwa ushapu wako wa kuelewa na utulivu wako wa akili. Hii ni mojawapo ya tip muhimu sana ya kuzingatia wakati unaongea na mwanamke. Kama wahenga wasemavyo, hata kaa hauna mwonekano mzuri, ushapu wa akili na uelewa kutamfurahisha moyo wake. Kumfanya acheke sana bila ya kujielewa, kutamfanya yeye apende kuongea na wewe zaidi na wakati mwingine atakupa namba ili muwe mnawasiliana hatakama mpo mbali.
#14 Jitahidi uwe na mwisho mzuri wa maongezi. Kukatisha maongezi yenu wakati bado anafurahia maongezi kutamfanya ajisikie vibaya, lakini usijali hii itamfanya apende kuwa na muda mwingine muwe pamoja.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger