Mambo vipi wapenzi wasomaji wa makala ya MAPENZI, namshukuru Mungu kuvuta pumzi ya leo, sio kila mtu alichaguliwa, na huu sio uwezo wala ujanja wangu bali Mungu mwenyezi.
Ukweli, wanaume wengi tumekuwa tukiteseka na janga hili la mapenzi kwa sababu ya kujikuta tunamaliza haraka tendo la ndoa na kuwaacha wenza wetu wakiwa na kiu kubwa ya mahanjumati.
Hili limefikia kiasi cha wanaume kuanza kuogopa ndoa au wake zao na wengine wakirubuniwa zipo dawa hizi na zile bila kupata suluhisho sahihi.
Poleni sana wenye tatizo hili na nataka kukuambia, ugonjwa huu unatibika! Kwanza napenda wewe msomaji mwanamume ambaye unapitia kurasa hii, uanze kufanya uchunguzi wa mwili wako kwa daktari, pima vipimo vyote hospitalini kubwa na sio za uchochoroni!
Unaweza kuanza kupima damu yako, kama damu yako imechafuka au kushambuliwa na vijidudu vya maradhi, ni wazi hata uwe mfanyaji wa mazoezi kiasi gani, bado tatizo la kuwahi kufika kileleni mapema litakuwepo.
Kumbuka damu ndiyo inayofanya kazi kubwa na kuujaza uume wako uwe imara, sasa kama damu imeshambuliwa na magonjwa kadhaa, ni wazi itakuwa dhaifu na wewe mwenyewe katika mapenzi pia utakuwa dhaifu kabisa!
Pia Soma
Hata unapokuwa na malaria sugu, uwezekano wa damu yako kuwa bora na kufanya mapenzi vizuri ni ngumu. Unapokuwa na ugonjwa wa ngozi hadi kwenye uume, vijidudu hushambuliwa uume wako na mshipa inayosambaza damu kutoka kwenye ubongo wako kwenda kwenye uume wako itashindwa kufanya vizuri.Sio jambo la utabiri hili, unapaswa kufanya ‘sevisi’ ya mwili wako kwanza. Acha kulialia kitandani na kumfanya mwanamke ajute kwa nini ameingia kwenye ndoa ya mateso.
Wakati mwingine wanawake wanaweza kukuambukiza magonjwa na yakawa sugu na kwasababu wewe lazima usimame na ufanye kazi zako, basi unapaswa kujitibu na kumtibu mkeo ili wote mwende sawa.
Kama alipata magonjwa ya zinaa, au yenye kushambulia ‘kalamu’ yako, basi wa kwanza kuteseka ni wewe mwanamume. Mwanamke hateseki kwa sababu hana uhitaji wa ‘kusimama’, hata akiwa amepoa, unaweza kumuingilia na ukamaliza haja zako bila tatizo lolote.
Ugonjwa wa kisukari nao ni shida nyingine kwasababu unashambulia damu, na ukumbuke kuwa damu yako inapokuwa dhaifu hata ‘kalamu’ yako itakuwa dhaifu pia.
Ukiwa na infection yoyote mwilini mwako, ni tatizo. Hivi wewe mwanamume unafanyia gari lako ‘sevisi’ kila mwezi, unashindwaje kufanya ‘ovaoili’ mwili wako? Kumbuka oil chafu inaweza kuua injini yako ya gari, hata katika mwili; kama tumboni una masalia kibao ya chakula ambayo yaliganda katika utumbo wako na yamekaa muda mrefu kwasababu kila siku unakula vyakula na kunywa vinywaji baridi, unategemea nini? Lazima utapata matatizo tumboni na ukumbuke kuna mishipa ya kumfanya mwanaume awe imara inayotokea tumboni.
Ndiyo maana unaona mtu mwenye ngiri anajikuta akishindwa kumpatia mkewe dozi zuri kwasababu ngiri inapooza uume na kuulaza kabisa.
WANAWAKE WANAVYOISHI NA WANAUME ZAO, NI SABABU YA KUSHINDWA KUPEWA VILIVYOBORA.
Jamani, hebu fikiria inakuwaje mwanamume anaweza kusimamisha kalamu yake? Ili uweze kusimamisha kalamu yako akili yako ina sehemu kubwa ya kazi katika kusababisha hali hiyo.
Acha mawazo ya kushindwa kusimamisha kalamu yako na badala yake jenga hisia nzuri kwa mkeo, leo utampatia kile roho yake inapenda. Wakati mwingine uoga wa kuhisi utashindwa unaweza kukusababishia kweli ukashindwa.
Pia kuna baadhi ya wanaume wameoa wanawake wakorofi na wakali muda wote ambao hawajui thamani ya mapenzi zaidi ya ubabe, hili nalo ni tatizo
0 comments:
Post a Comment