juu

Tuesday 5 November 2019

Mwanaume fahamu Anachohitaji mkeo kwa wakati huo ni MTU ANAYEMTEGEA SIKIO.

Brother
Mkeo anakuhitaji. Hawezi kutembea kwenye safari ya maisha yake akiwa peke yake. Anapoanguka, anahitaji umshikilie na umsaidie kusimama. Anakuhitajia uyafute machozi yake na kumkumbatia barabara. Anahitaji umfariji pindi maisha yanapokumbwa na dhoruba kali.
Ninafahamu kuwa wewe ni mume mzuri sana, tena mzuri kabisa. Hakika mkeo amebarikiwa sana kuwa na mume kama wewe.
Miongoni mwa mambo unayoweza kumsaidia mkeo kupata nguvu na kurejesha nishati yake pindi anapozidiwa na mambo au kukandamizwa na msongo wa mawzo ni KUMUACHA AZUNGUMZE ATAKAVYO.
Wakati fulani njia bora kwa mwanamke kukaa sawa ni kueleza mawazo na fikra zake zote. Muache mkeo azungumze hisia na matatizo yake yote yanayomsibu.
Muoneshe huruma, msikilize vizuri, uliza maswali kwa njia nzuri. Shiriki kikamilifu katika mazungumzo yake. Muache aseme, wala usihofu, mpe hiyo nafasi asafishe moyo wake.
Wakati mwingine anaweza hata akalia, usiogope, mruhusu ausafishe moyo wake kikamilifu, mnyamazishe taratibu na kwa maneno ya faraja: “Pole mke wangu, pole malkia wangu, pole kipenzi changu, usilie, usihofu niko hapa pamoja nawe nk.”
Anachohitaji mkeo kwa wakati huo ni MTU ANAYEMTEGEA SIKIO. Huo ndio msaada anaoutaka kutoka kwako.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger