juu

Friday, 15 November 2019

Unapoanza mahusiano mapya Usithubutu kumwambia haya mpenzi mpya




Mapenzi huwa ni matamu sana mwanzoni na hii huwa inatokana na kila mtu kuexperience kitu kipya kutoka kwa mwenzake ambaye hakuwa naye awali.

Mambo mengi huwa mazuri na matamu kutokana na ukweli kwamba kila mtu hujitahidi kumfurahisha mpenzi wake mpya, Kila mmoja hujitahidi kuficha tabia zake mbaya ambazo zinaweza kumkera mwenzake katika uhusiano mpya.

lakini mtu huwa hawezi kuishi kwa muda wote katika hali ya kuficha tabia zake ndiyo maana huwa inafikia kipindi mtu anaanza kuona hapendwi tena lakini siyo kweli kipindi cha kujificha tabia kinakuwa kimeisha na mtu huanza kuishi maisha yake halisi kama si mtu wa kupiga simu ataacha kuwa anapiga kama anahasira basi atazionyesha wazi wazi.

Basi point yangu kubwa ni nini? Point kubwa hapa msomaji wa Wakubwa Wanafaidi App ni kwamba unapoanza uhusiano na mrembo au mkaka mpya jitahidi usimwambie mambo mengi mpenzi wako mpya kuhusu X wako.

Kulingana na maelezo niliyokupa mwanzoni faida ya kutomwambia mpenzi wako tabia za mpenzi wako wa zamani itakusaidia sana kutoharibu kwenye huo uhusiano mpya.

Mfano chukulia unaanza kumwambia mapungufu ya X wako mpenzi wako mpya kumbe naye hayo mapungufu anayo ila kwakuwa ni mwanzo anajitahidi tu kuyaficha.

kama ikitokea unamwambia mambo ambayo hata yeye anayo na ukawa unamwelekeza kuwa ndiyo sababu ya kuachana kwenu basi hata huyo mpya ataona na yeye utamuacha hivyo hawezi kuwa serious tena na wewe akiamini mtaachana kutokana na mapungufu yaliyosababisha mkaachana na X wako na yeye anayo.

Nakushauri kutokuwa unayataja mapungufu ya X wako bali lenga zaidi kwenye mahusiano yako mapya naongelea zaidi kuhusu mipango yenu na kujipanga kukabiliana na mapungufu ya Mpenzi wako mpya.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger