juu

Tuesday, 5 November 2019

Zifahamu faida za kukusahau na kusamehe mpenzi wako wa zamani



Una hasira, una uchungu, una maumivu makali katika moyo wako, unatamani kulipa kisasi, unatamani kumuacha, unatamani kupata mtu anayekupenda na kukujali ili aumie! Je, ukimuacha hasira yako itaondoka, na je, inawezekana kupata mwingine ambaye mtaishi bila kukoseana pasipo jitihada zozote?

Ngoja nikwambie kitu, mahusiano mazuri yanatengenezwa. Hasira, uchungu na kisasi vinakutafuna na havitakuacha salama. Kilichopo ndani lazima kitajidhihirisha nje na bila shaka utapata magonjwa usostahili. Hakika nakwambia, huwezi kutengeneza ukiwa na chuki, hasira na uchungu vitu hivyo ni lazima vitajidhihirisha ktk matendo yako. SAMEHE kwaajili ya Mungu wako, samehe kwaajili ya afya yako, samehe kwaajili ya furaha yako, samehe kwaajili ya future yako, samehe saba mara sabini, samehe na utengeneze furaha yako upya.

Mungu hawezi kukupa mtu wa kukupenda ili ulipe kisasi, kisasi si cha mwanadamu, kisasi ni cha Mungu. Na hatakaa akupe kwasababu hujui kusamehe ni UTII. Samehe na mwachie Mungu atengeneze, kama moyo wake anaufanya kuwa mgumu basi kisasi cha Mungu ki mlangoni kwake.

Sio rahisi kusamehe kama umebeba uchungu mwingi, mwambie Mungu akusaidie na kukufundisha kusamehe. Inachukua muda lakini usijali kwamaana kadiri unavyosamehe ndivyo unavyojiponya.

Hasira na uchungu ni sawa na saratani inayosambaa ndani ya mtu kidogo kidogo, inaathiri nafsi yako na mwili wako. Maandiko husema, “usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, maana hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu. Mwenye kutunza hasira ni mpumbavu kwamaana hasira inamdhuru yeye na si aliyekasirikiwa”.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger