juu

Tuesday 5 November 2019

Mtu asiye na penzi la kweli, utamgundua tu mambo haya



Kuna muda unaweza ukawa unajipa moyo kwamba, kuna siku uhusiano wako utakuwa sawa na mwenza wako atatulia kama ilivyo awali. Kimsingi mtu asiye na penzi la kweli, utamgundua tu mambo kadha wa kadha. Kwa mfano mpenzi wako anakuwa mgumu wa kuonana na wewe, mawasiliano duni, msiri sana, hakujali, haoni hatari kukueleza kwamba muachane, haoneshi kukupenda kiivyo, hafikirii kukutamburisha kwa rafiki na ndugu zake na mara nyengine hupajui kwake au kwao, huyu ipo siku atakuacha na kukuumiza sana.

Kimsingi hutakiwi kulilea penzi lisilokuwa na muelekeo chanya, usikubali kulizwa, unapoona nyendo za mwenza wako hazikuridhishi, chukua uamuzi wa haraka wa ku_move on huku ukiamini kwamba utampata mwingine mwenye nia ya dhati juu ya maisha yako.

Sasa kwanini usichukue hatua za haraka za kumuondoa kwenye maisha yako? Kuna raha gani ya kuwa na uhusiano na mtu asiyekupa raha ya maisha badala yake ni mtu wa kukufanya uwe na majonzi kila wakati?

Usikubali kuwa mtumwa wa mapenzi kwa kukubali kuburuzwa na mtu unayeweza kumuacha na maisha yako yakaendelea kuwepo. Amini wewe ni mzuri, beautiful au handsome na una kila kigezo cha kupata penzi la uhakika na lenye tija si la kubabaisha.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger