juu

Tuesday 5 November 2019

Nawezaje kuwa wa mvuto?– How to be Hot guy.

Mvuto katika mapenzi huwa katika macho ya mtazamaji. Kuna watu tukiwaona wanatuvutia na wengine hawakushtui kwa lolote mana kwako hawana mvuto kabisa. Japo ndiyo, kila mtu ana vigezo vyake, na hiki ndicho kinachofanya mapenzi kuwa kitu cha ajabu, kitu kidogo tu kwako kinaweza kuwa kivutio kikubwa kwa wanawake.

Hatua za kuwa na mvuto: Kanuni 20 za kufata kuwa HOT!..

Kama unataka kuwa na mvuto katika macho ya wanawake, unatakiwa uzifate hizi kanuni “kali” 20. Kumpata mwanamke wa ndoto zako, unatakiwa ufanye kitu cha ziada na uache ndoto za mchana.
#1 Vaa Rasmi. Jitahidi kuwa smart kwa kuvaa nguo za
kitambaa(suruali na shati), unaweza vaa kadet lakini usipende sana kuvaaa jeans. Haimaanishi kuwa wanawake hawapendi jeans, lakini unatakiwa uonekane kuwa ni mtu unayejitambua kimavazi(be formal). Kumbuka maavazi humpa mtu heshima na humvunjia mtu heshima pia.
#2 Chezea vifaa vya muziki. Hata kama haujui sana, jitahidi ujifunze kidogo unapokuwa na muda mana kwanza, inakuongezea ujuzi wa vitu vipya ambavyo ulikua hauvijui, lakini pili wanawake hupenda na hutilia sana maanani vitu vidogo vidogo kama hivyo. Jifunze kuchezea gitaa(guitar), kenanda(keyboard), zeze, n.k.
#3 Kuwa Gentlemen(Simple). Hakuna kitu kinawavutia wanawake kama mwanaume anayewaheshimu. Mwanaume mwenye mvuto ni yule anayetufungulia milango, kutuvutia kiti ili tukae, na kutuagizia kitu cha kula / kunywa pale ambapo hata hatujui tuagize nini. Kumjali mwanamke sio ujinga, ni point kubwa ya kutufanya tukupende.
#4 Jitahidi kujua vitu anavyopenda. Mathalan rangi anayoipenda, wimbo anaoupenda sana, na wakati mwingine uwe na uwezo wa kulitaja jina lake kamili(majina matatu).
#5 Vaa unique. Nenda hata kwenye duka wanalouza nguo / mavazi ya kizee, usipende sana kufanana na wenzako mana hautaonekana tofauti na wenzako. Wanaozitengeneza hizo nguo wana sababu zao zinazowafanya kuzitengeneza kizazi hata kizazi.
#6 Mzuzu(Mchebe) siyo ishu. Ndevu ndefu ni kwa wale watu wa itikadi kali tu, lakini kwa getlemens sio tabia yao kufuga. Unaeza ukafikiri utavutia sana, lakini unaweza kuwa unaficha uzuri ulokuwa nao. 
#7 Kuwa mcheshi kidogo. Hakuna kitu kinachotuvutia sisi wanawake kama mwanaume anayeweza kukuchekesha au kufanya vitu ambavyo vinaweza kukuondolea mood mbaya uliyokuwa nayo. Kama wewe ni mtu unayeweza kuchekesha, jitahidi kufanya hivyo kadri uwezavyo. Wanaume wakimya au wakali au serious mda wote wanakera sana na hawavutii. 
#8 Kwenda na wakati ni sawa, lakini kuwa mwathirika wa mitindo ni kitu kibaya. Kama kuna mtindo mpya umekuja uchinguze kama unaendana na kanuni zako na style yako, chukua kilicho kizuri na cha kukuletea heshima na achana na vitu ambavyo siyo vya msingi. Mitindo mingine waachie vibaka wa mtaani(You want to be gentlemen right?).
#9 Jitahidi unukie. Kuwa na perfume nzuri au spray ambayo siyo kali sana. Itakufanya uonekane unajijali, na hivyo utawapiku wanawume wengine. Kama hauwezi kuchagua mwambie msichana akuchagulie.
#10 Kuwa mtu wa fashion sana inaboa, lakini kuwa msafi nikitu kikubwa. Tunapenda mwanaume ambaye hatakama hana nguo nyingi lakini awe msafi na azifue nguo zake mwenyewe na aweze kuzipangilia. Kama hauwezi kupangilia mtafute mtu akusaidie.
#11 Kuwa mwerevu(Be intelligent). Wanawake sikuzote hawapendi wavulana – hupenda wanaume, tunahitaji kitu cha ziada zaidi ya sura nzuri ili kujua mwanaume huyu anavutia. Kama mwanaume ataonekana kuwa na mvuto lakini muda wote akawa anafungua domo na kila saa utasikia “duh,”, au kuwa na utani usiokuwa na msingi, atapoteza mvuto wake dakika 0. 
#12 Lazima unyoe vizuri. Kama unadhani wanawake tunapenda nywele rafu-rafu kama vile umetoka kitandani, fikiri tena. Haimaanishi hatupendi nywele ila tunapenda ukamilihe uzuri na usafi wa mwili wako ambao Mungu alikupa. Chagua mtindo mzuri wa nyele usiwe wa kihuni.
#13 Mazoezi ni muhimu. Ukweli ni kwamba sisi wanawake huwa tunaiangalia miili yenu kama mnavyoiangalia yetu. Haimaanishi kwamba tunapenda wanaume wenye vifua vikubwa hapana, tunapenda mtu mwepesi na mwenye mwili unaoonekana kuwa na afya.
#14 Tabasamu la Furaha. Kununa siyo kivutio kwetu. Tunampenda mwanume anayekuwa na furaha na mtu yeyote anayekuwa naye. Hakuna kitu kinachovutia kama mwanaume anayeweza kucheka kwa nguvu bila ya kujali / kuogopa.
#15 Jiamini. Kama unataka kuwa na mvuto, jiamini, hatakama kundi kubwa la watu litakuwa kinyume na wewe usibadili msimamo wako. Hii inakutofautisha na wengine na hicho ndicho tunachokihitaji(mwanaume mwenye utofauti na wengine).
#16 Siyo kila mwanaume anayeweza kubeba vyuma vizito vya kilo 300. Tunapenda mwanaume anayetufanya tujisikie salama na kulindwa.
#17 Jikague kabla haujatoka. Tunapenda mwanaume mwenye tabia ya kujikagua kabla hajatoka. Kujiangalia kwenye kiyoo tangu kwenye unywele mpaka kwenye kiatu. Usipende kurudia rudia nguo. Mwanaume anayjali muonekano wake hakosi points kwetu.
#18 Macho. Kuna kitu cha tofauti sana pale unapomtizama mwanamke machoni. Kama unaweza kumwangalia machoni bila kupepesa macho, ataweza akapata picha wewe ni shujaa kiasi gani na utamvutia sana. 
#19 Tembea vizuri. Usijaribu kuiga mtu anavyotembea. Tembea kiheshima wakati wote na uhuni weka pembeni. Usidunde kama kitenesi, utaonekana kituko.
#20 Weka uwiano kati ya kusikiliza na kuongea. Unaonekana sana kuwa mtu wa tofauti pale unapoweza kubalance mazungumzo yako. Mwanamke wako anapenda kukusikiliza ndiyo lakini ni endapo tu anataka kukusikiliza. Jitahidi kumpa na mwenzio muda wa kuongea pengine ana mengi ya kukuambia. Hiyo inatufana tujione na sisi kuwa wa muhimu na kuthainiwa.

Hivyo mtu wangu usipoteze muda, kama ulikua unaonekana kituko ni vile ulikua haufati hayo mambo. Jitahidi sasa kuzitumia hizi tips zitakusaidia.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger