juu

Friday, 15 November 2019

Huu ndio ukichaa wa mapenzi

Related image🔵Kushika mimba ukadhani ni mtego ili uolewe.
🔵 Kutafuta mkamilifu wakati tabia zako tunakuvumilia tu.
🔵 Kutafuta msichana mrembo wakati huna pesa.
🔵 Kutafuta mke mwema kanisani wakati we unaenda kanisani wakati wa maombi ya Christmas tu.
🔵 Kusema wanawake wote sawa.
🔵 Kuendelea kuchagua wanaume wakati unajua waoaji siku hizi wachache.
🔵 Kuishi na mpenzi wako kabla ya ndoa, unamfulia, unampikia na unampa penzi wakati unajua hujulikani kwao, ukiachwa unatafuta ushauri mitandaoni.
🔵Kusema umeokoka lakini unazini na mchumba kama kawaida kwa kisingizio kwamba soon mtakuwa mke na mume!
🔵Kuogopa kuongozana na msichana au mvulana eti mtaingia majaribuni, unajua kutamani tu ni uzinzi?
🔵 Kufikiri kwamba utampata mtu mwenye sifa mia nane unazozitaka labda umuumbe mwenyewe!
🔵Kujifanya unapendwa wakati moyoni unajua wazi mtu kakuchoka, na amekwambia kabisa anatafuta mtu mwingine!
🔵 Kumhonga mwanaume ili akuoe!
🔵 Kudhani kwamba kutoolewa ni laana, hii ni bangi mbaya!
🔵 Kumtongoza mchumba au mke wa rafiki yako!
🔵 Kuoa wakati huna kazi /chanzo cha kipato!
🔵 Kufikiri eti wanaume wa kiafrika wanaweza kufanya mambo ya kwenye tamthiliya za kifilipino.
🔵 Kumsomesha mtu ili uje umuoe!
🔵 Kumng'ang'ania mtu asiyekupenda, utazimia ukialikwa harusini!
🔵Kuwaeleza mashosti zako 'utam' anaokupa mtu wako!
🔵 Kumwambia bebi wako anunue gari wakati amepanga chumba kimoja……..
Nimeipaste kama ilivyo kama imekugusa Nivumilie
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger