juu

Monday 25 November 2019

Kwanini ndoa Nyingi huvunjika mapema




Mpenzi msomaji wa makala zetu pendwa napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha tena katika safu hii ya Mapenzi na mahusiano. Kama ndio umepakua Application Hii leo hujachelewa, Bado mambo ya kujifunza ni mengi sana.

Tumekua tukiona ndoa nyingi sana duniani zikifungwa kwa mbwembwe kubwa mno kiasi kwamba wawili hao hawatakuja kuachana. La hasha! Sikweli. Leo nakuletea siri kubwa zinazopelekea ndoa hizo hizo unazoona hazitakufa kuvunjika kwa haraka.

Moja kwa moja sipendi kuwachosha sana Huwa nawaletea TIPS hizi zipo wazi kabisa naimani utagungua mapungufu na changamoto za ndoa zilivyo.

1.Kwa sasa hakuna Mapenzi bali kuna biashara ya mapenzi, Kwanini nasema biashara ya mapenzi sasaivi watu wanaangalia maslahi kwanza then mambo mengine baadae hivyo kama huna pesa gari na nyumba lazima uachwe tu.

2.Wanawake kujitambua. Sasa hivi sio kama enzi za nyuma, wanawake wengi wameelimika hivyo kuwa na ufahamu wa kujua haki zake kama mwanamke ila wanawake wa zamani wengi walikuwa hawapelekwi darasani hivyo haki nyingi za mwanamke zilikuwa zimejifunga hazijulikani. Mwanamke wa zamani alikuwa anajua kuwa ni haki yake kupigwa, kuonewa na mwanamme ila wa sasa hivi baada ya kuelimishwa na sheria kufuata mkondo wanawake wengi wameamka. Nafasi ile ya mwanamke kuvumilia kipigo imekuwa hakuna tena hivyo akikutana na mwanamme huyu mwenye tabia ambayo inavunja haki za mwanamke anajua jinsi ya kujitetea na hivi ndivyo wanaume weengi hawapendi na kupelekea ndoa kuvunjika.

3. Wanawake wa nyuma wengi walikuwa ni golikipa akae nyumbani asubiri mume ndio amuhudumie kifedha na matumizi ila wanawake wa sasa wengi ni watafutaji hivyo kupelekea yale manyanyaso ya wanaume waliyokuwa wakiwapa wanawake kisa ni kumhudumia sasa mwanamke hakubali. Mwanaume alikuwa anauwezo wa kufanya lolote kwa mkewe kwa gia ya kwamba atamnyima fedha za chakula n.k. hivyo mwanamke alikuwa hana budi awe mpole asikose anavyohitaji yeye na watoto.

4.Kutokana na Biashara za Kimataifa, Utandawazi wanawake na wanaume wamekuwa wakiiga tabia za Magharibi na za nchi nyingine sababu kwa sasa imekuwa ni rahisi sana kumuona Rihana msichana mrembo kavaa nini, je kapendeza kuliko enzi hizo ulikuwa huwezi ona picha wala video hizi kwani hata luninga ilikuwa unalipia sehemu kuangalia, Simu za mkononi zenye mtandao hakuna hivyo utakayemuona hapo karibu Role model wako anakuwa ni jirani yako au mtu katika Familia yako.

5.Sasa hivi wanawake na wanaume wamekuwa wakishiriki sana katika tendo la ndoa kabla ya kuoa na kuolewa. Hivyo pale anapoingia katika ndoa hakuna jipya analoenda kuliona. Ila enzi za nyuma ilikuwa mume na mke mnaowana bado hata tendo la ndoa hamjakutana. Mume ndio kwaanza anayemvunja bikira mkewe na kupelekea kuwa na mapenzi moto moto, kuona kitu kigeni ndani ya miili yenu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger