juu

Sunday 24 November 2019

SHEMEJI HIYO MITEGO YAKO DAWA YAKO IKO JIKONI WE HAYA

Katika maisha yangu napenda sana amani ndio maana huwa najisikia vibaya sana ikitokea nimemkwaza mtu wangu yoyote wa karibu kwani najiuliza atanisamehe kweli kwa hili kosa 

nililomfanyia? Historia ya maisha yangu imenifanya niwe na moyo huu wakutopenda kumkwaza mtu kwani nimefadhiliwa sana na kaka yangu,nimepewa kila kitu muhimu ambacho kijana anastahili awe nacho kama vile simu nzuri,pesa ya matumizi achilia mbali ada ya masomo ya shule za private nilizosoma kuanzia kindergarten mpaka nimefika chuo kikuu,

Kwa kweli kaka yangu ni mtu wa pekee sana maishani mwangu na hakika siwezi kulipa fadhila zake. Ameniamini sana kiasi cha kuwa ananiachia gari lake anaposafiri niwe huru kulitumia muda wowote nitakao lakini kwa bahati mbaya moyoni nimekuwa mwenye huzuni sana kwani mke wa kaka yangu yaani shemeji amekuwa tatizo kila kaka akisafiri maana vituko anavyonifanyia sio siri nahisi 

kutamani kuhama kwake pasipo hata kujua nitaenda wapi. Shemeji anathubutuje kunitolea chozi akinililia eti anataka awe na mimi kimapenzi wakati unajua fika kwamba hili si jambo linalokubalika hata kidogo,hakika shemeji uzuri wake anautumia kama chambo cha kutaka kuninasia, zaidi ni pale anapokuwa anavaa vinguo ambavyo ni robotatu uchi tena unategea tukiwa wawili tu nyumbani. 

Hakika siwezi kulipa ubaya kwa wema kwani kaka yangu ndiye tegemeo langu na furaha yangu,yeye wala hajali hilo labda kwa kuwa anajua fika kwamba kaka anampenda sana na hawezi kuamini neno lolote aambiwalo kuhusu yeye,kwanini lakini wataka kuharibu undugu wetu mimi na kaka yangu? 

Shemeji afanye lingine lolote ila suala la kutaka nifanye ngono Hapana, shemeji ananikosesha raha ya maisha kwani amekuwa king’ang’anizi isivyokawaida mpaka baadhi ya majirani wameanza kuhisi kitu. Amefikia pabaya sasa shemeji that’s not fair at all please give me a break. Tafadhali unaushauri gani kwa huyu kijana aliyeandika waraka huu ambaye kwa kweli anatatizo hili sugu ana shindwa afanye nini?Toa ushauri wako uwe msaada kwake.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Translate

sam magelle

Main Menu Links

HABARI KALI ZAIDI

HABARI ZILIZOPITA

CHAGUA HABARI na sammagelle.com

Copyright © juu | Powered by Blogger